MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Nov 3, 2015

Utambulisho wa kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili Washington DC

Mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza (katikati) akizungumza na Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi waTanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme na baadhi ya waliohudhuria uzinduzi huo
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme (wa pili kushoto) ambaye pia alimuwakilisha Mhe Balozi Wilson Masilingi, akimsikiliza mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza
Steven Mghaza akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa kwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi, na mwakilishi wa balozi kwenye hafla hiyo, Swahiba Mndeme,Kushoto ni Meneja mauzo wa CBC Radio R.J Trzaska, mratibu wa Mis Congo na msanii toka congo
Mshereheshaji wa siku hiyo, Grace Ssebo akikaribisha wageni.
 
Jumamosi,Oktoba 31, Swahili Media Network LLC kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC walitambulisha kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili JAMBO TV SHOW kitakachoonekana kwenye kituo cha Televisheni cha DCTV hapa Marekani.

Pia, Swahili Media Network inaandaa kipindi cha Radio cha Jambo America, kinachosikia kupitia WJFK ambayo ni radio-dada ya WPGC chini ya shirika la CBS Radios.