Majeruhi wakikimbizwa hospitali.Polisi wakiwasaidia waathirika wa tukio hilo.
Umati wa watu kabla ya tukio hilo.
Umati wa watu kabla ya tukio hilo.
Hali ilivyokuwa eneo la tukio. Polisi wakiimarisha ulinzi. …Pakiwa pamepooza.
New Orleans, Marekani
WATU wapatao 16 wakiwa kwenye mkusanyiko
wamejeruhiwa baada ya kufyatuliwa risasi na watu wasiojulikana mjini
New Orleans nchini Marekani.
Tukio hilo limetokea jana jioni amapo
watu wapatao 500 walikuwa wamekusanyika kwenye makundi mawili katika
bustani ya Bunny Friend Park mjini New Orleans. Kundi la kwanza
walikwenda kutazama video iliyokuwa ikiandaliwa bustanini hapo, na kundi
la pili wakienda kwenye gwaride la wakazi wa mtaa huo ndipo kikundi
kingine cha watu watano wasiofahamika wenye silaha akiwemo mwanamke
mmoja walizuka na kuanza kuwashambulia umati huo kwa kuwarushia risasi
kisha kujeruhi 16.
Baada ya taharuki hiyo polisi wa eneo
hilo walifika na kuanza kujibizana nao risasi ndipo wakaamua kukimbia,
polisi waliwachukua majeruhi hao na kuwapeleka hospitali.
Shuhuda mmoja wa tukio hilo amekaririwa
akisema kuwa, mmoja kati ya wavamizi hao alijipenyeza katikati ya umati
huo na kufyatua risasi mara 10, baadaye waliingia watu wanne wakiwa na
silaha pia, nao wakaanza kushambulia umati huo.