MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 14, 2015

Benki ya Exim yakabidhi gari kwa mshindi wa kampeni yake ya akaunti ya malengo

Meneja Bidhaa wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Aloyse Maro (kushoto) akikabidhi mfano wa ufunguo wa gari kwa Meneja Mahusiano Msaidizi wa benki hiyo Bi. Naomi Sanga (katikati) ambaye alimuwakilisha mshindi mkuu wa kampeni ya akaunti ya malengo ya benki hiyo aliyejishindia gari aina ya Toyota IST kwenye hafla fupi ya makabidhiani iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Anaeshuhudia ni Meneja Masoko wa Benki hiyo Bw Abdulrahman Nkondo.

Benki ya Exim Tanzania imekabidhi zawadi kuu kwa mshindi wa kampeni ya akaunti ya malengo baada ya kuendesha droo yake ya mwisho na kubwa chini ya usimamizi wa Bodi ya taifa ya michezo ya kubahatisha (GBT) jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Bi. Naomi Sanga ambaye ni Meneja Mahusiano Msaidizi  wa benki hiyo alikabidhiwa funguo za gari aina ya Toyota IST kwa niaba ya mshindi katika hafla fupi ya makabidhiano iliyoandaliwa na benki hiyo na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ushindi huo wa mteja wao huyo Bi. Sanga alielezea furaha yake na kusema kuwa mpango wa Benki ya Exim wa kuwazawadia wateja wake unaonyesha shukrani za benki hiyo katika kutambua uaminifu na mchango wa wateja wao.

"Mshindi wetu ameupokea ushindi huu kwa furaha kubwa japo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake alishindwa kujumuika nasi leo. Ubora wa bidhaa za Benki ya Exim, huduma bora kwa wateja na viwango vinavyovutia vya riba vinavyotolewa katika akaunti hii ya malengo vinathibitisha dhamira ya benki hii katika kukidhi mahitaji ya wateja wao,” alisema.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Meneja bidhaa wa Benki ya Exim, Aloyse Maro, aliwapongeza washindi waliojizolea zawadi mbalimbali katika kipindi chote cha kampeni hiyo huku akiwashukuru wateja waliojitokeza kushiriki katika droo hiyo.Kwa mujibu wa Bw. Maro, sambamba na zawadi hizo kampeni hiyo iliambatana na utoaji wa riba nzuri zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti hiyo ya malengo.Alisema lengo la benki yake ilikuwa kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa Watanzania.

“Hii ni moja ya njia za benki hii kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini ili kuongeza tija katika maendeleo ya taifa,” alibainisha.

chanzo : JIACHIE