CHINA YASAIDIA VITANDA 60 VYA KUJIFUNGULIA WAKINA MAMA KWA MKOA WA LINDI
Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akiangalia baadhi ya vitanda
ambavyo vimekabidhiwa kwa mkoa wa Lindi kwenye hafla fupi iliyofanyika
kwenye hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia)
akiangalia vitanda hivyo vya kujifungulia wakina mama akiwa pamoja na
Katibu Mkuu wa Taasisi ya kukuza Urafiki wa Tanzania na China Ndugu
Joseph Kulwa Kahama.
Bi.
Ziada Maulid akitoa shukrani zake mbele ya Balozi wa China nchini Dk.
Lu Youqing mara baada ya ya Balozi huyo kukabidhi vitanda 60 vya
kujifungulia wakina mama.
Balozi
wa China nchini Dk. Lu Youqing pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama
wakiwasili katika kata ya Kiwalala, jimbo la Mtama tayari kwa kukabidhi
vifaa vya matibabu katika Zahanati ya Mauhumbika.
Wakazi wa kijiji cha Mahumbika wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya vifaa vya matibabu katika Zahanati yao.
Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akihutubia wakazi wa Mahumbika
ambapo pamoja na kuahidi misaada zaidi ikiwemo kwenye matatizo ya maji,
Balozi pia aliahidi kusaidia vijana wanaomaliza Chuo Kikuu kwenda
kujiendeleza nchini China.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam
za shukrani kwa Serikali ya China kwa msaada wa vifaa vya tiba
vilivyogharimu zaidi ya milioni 20.
Balozi
wa China nchini Dk. Lu Youqing akizungumza kabla ya kukabidhi vitanda
60 vya kujifungulia wakina mama katika mkoa wa Lindi, kushoto ni
mkalimani wake Ndugu Mu Lin.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB)
akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ambapo alisema Serikali ya China pamoja na
watu wake wamekuwa marafiki wa kweli kwa Tanzania na wamekuwa wakitoa
misaada mingi bila kutoa masharti.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB)
akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ambapo aliishukuru Serikali ya China pamoja na
watu wake kwa msaada wa vitanda 60 vya kujifungulia ambavyo vitasaidia kuokoa maisha ya Mama na Mtoto katika mkoa wa .
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI