MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 17, 2015

MHAGAMA: AZITAKA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUTEKELEZA MAELEKEZO YA SERIKALI YA KUJIAANDAA NA KUKABILI MAAFA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akiangalia Sehemu ya mtaro wa maji katika eneo la Tegeta, Basihaya wilayani Kinondoni, Jijini Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mkazi wa Tegeta, Basihaya Jijini Dar es Salaam, Jumanne Malongo alipokuwa akimueleza jinsi wembamba wa mtaro huo unavyosababisha maji kujaa katika makazi yao, leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. 
 Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manisipaa kinondoni, Ando Mwakunga akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), uharibifu wa “kalvati” katika eneo la Boko, Ununio Jijini Dar es Salaam, leo wakati Waziri huyo alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo.