MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 10, 2015

MWIGULU AWASHUKURU WATANZANIA NA RAIS WA TANZANIA

Namshukuru Mungu kwa yote anayoendelea kunitendea katika Maisha yangu,
Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.J.P.J.Magufuli kwa kuniteua kuwa Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Nawashukuru Watanzania kwa maombi na ushirikiano mlio na mnaoendelea kunipa katika kila hatua ya maisha yangu.

Naishukuru familia yangu(Mke wangu Neema Mwigulu,Watoto wangu Joshua,Gracious na Isack) Wazazi,ndugu na jamaa kwa kuwa bega kwa bega kila hatua ninazopitia katika maisha yangu.
Naamini na nipo tayari kulitumikia Taifa langu kwa Uzalendo wa hali ya juu kama ilivyo desturi yangu,Nawaomba Watanzania mnipe ushirikiano wenu wakati wote wa Utekelezaji wa majukumu haya ya kulijenga Taifa.
Naahidi sita WAANGUSHA.
Mungu Ibariki Serikali yetu,
Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
HAPA NI KAZI TU

chanzo:Facebook