MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 6, 2015

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akutana na Rais wa China, atunukiwa Heshima ya Companion Award na Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM), aongoza ujumbe wa AU Comoro

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Rais wa China, Mheshimiwa Xi Jinping pembezoni mwa Mkutano wa Africa na China unaofanyika Johannesburg , Afrika Kusini. Waliosimama pembeni ni Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania, Rais Thomas Boni Yayi wa Benin, Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
----------------------------------
Taasisi ya Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM) inayojishughulisha na kukuza ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia kwa nchi za Jumuiya ya Madola, imemtunuku Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha ukuaji wa matumizi ya sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu. Rais Mstaafu Kikwete, alikabidhiwa Tuzo hiyo tarehe 1 Desemba, 2015. 
Taasisi hiyo yenye makao makuu yake London ndio inayoendesha Midahalo ya Kimataifa maarufu kama Smart Partnership Dialogue. Mkutano wa mwisho wa aina hiyo ulifanyika Dar es Salaam mwaka 2013 ukiwa Na kali mbiu ya "Kutumia Teknolojia Kuchochea Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Barani Afrika". 
Rais  Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Cheti cha Kumtunuku Yeshima ya Juu ya CPTM (Companion Award). Aliyesimama kushoto kwa Rais Mstaafu ni Dkt. Tan Sri Omar, Mwenyekiti wa Bose ya Wakurugenzi wa CPTM na pembeni yake ni Dkt. Mihaela Smith, CEO wa CPTM. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London.Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani baada ya kutunukiwa tuzo ya  heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliteuliwa na Mama Nkosamana Dlamini Zuma kuwa Mjumbe Maalum wa AU Comoro.  Mhe. Kikwete alikwenda Moroni, Comoro tarehe 30 Novemba, 2015 kufanya mikutano na wadau wa siasa kuhusu mgogoro wa kisiasa unaonukia nchini humo kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika April, 2016