MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Dec 22, 2015

Wafanyakazi wa Zantel wafanya sherehe za kufunga mwaka

      Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akitoa hotuba fupi ya kuzindua sherehe ya kufunga mwaka kwa wafanyakazi wa Zantel iliyofanyika mwisho wa wiki.
     Mkurugenzi Mwendeshaji wa Zantel, Bertrant Lacroix akijihudumia chakula wakati wa sherehe ya kufunga mwaka ya Zantel. Anayemfatia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Progress Chissenga.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wakati wa sherehe ya kufunga mwaka kwa Zantel.
 Mkurugenzi wa Rasirimali watu wa Zantel, Bi Joanita Mrengo akizungumza wakati wa sherehe ya kufunga mwaka kwa wafanyakazi wa Zantel.
 Mshauri wa Masuala ya serikali wa Zantel kwa upande wa Zanzibar akizungumza wakati wa sherehe ya wafanyakazi iliyofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort. 
 Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel wamefanya sherehe za kufunga mwaka zilizofanyika katika hotel ya Double Tree mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo pia wafanyakazi wa kampuni hiyo upande wa Zanzibar wamefanya sherehe za kufunga mwaka katika hotel ya Zanzibar Beach Resort.

Akizungumza wakati wa sherehe hizo Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin, amewapongeza wafanyakazi wote wa Zantel kwa ubunifu na uchapakazi waliounyesha katika kampuni hiyo.

‘Nawapongeza sana wafanyakazi wa Zantel kwa uchapakazi na ushirikiano waliounyesha kwa mwaka huu mzima, hasa katika maeneo ya huduma kwa wateja na ubunifu wa bidhaa mpya’ alisema Janin.