Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishiriki na Wananchi, Vikundi ya vya usafi wa mazingira pamoja na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafi wa mazingira hapo Kwahani Uwanja wa Farasi ikiwa ni kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Balozi
Seif akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira Mwenyekiti wa Kikundi cha
Usafi wa Mazingira cha Kilimani { Kilimani City } Nd. Khamis Shaali
Chum { mwenye T. Shirt Nyeupe }vilivyotolewa zawadi na Ofisi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira.Kushoto ya
Mwenyekiti huyo wa Kilimani City ni Mkurugenzi Maingira Nd. Juma Bakari
Alawi na wa kwanza kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja.
Baadhi
ya wapiganaji wa Vikosi vya ulinzi wakishiriki zoezi la usafi wa
mazingira katika Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi kuanza kwa shamra
shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka
52. Picha na – OMPR – ZNZ.
```Watendaji
wa Baraza la Manispaa Zanzibar wakijumuika pamoja na Wananchi na Vikosi
vya Ulinzi kwenye usafishaji wa mazingira hapo Mtaa wa Kwahani Uwanja
wa Farasi Mjini Zanzibar.`