Baraza
la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya
kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi
wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani
hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.
Akitangaza matokeo hayo leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji
wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi
zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili
kuboresha kiwango cha ufaulu.
Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na
asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya
A,B,C,na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za
ufaulu usioridhisha.
Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi
katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu
kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wawasaidie
kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri.
==>Bofya Hapa Kuyaona Matokeo