BEYONCE APONDWA JUHUDI ZA KUTENGENEZA FILAMU YA MWANAMAMA WA KIHISTORIA AFRIKA.
Mapema
mwanzoni mwa wiki hii magazeti nchini Afrika ya Kusini na baadhi toka
nchini Uingereza yamelalama na kutupa madongo ya kejeli kwa mwanamuziki
Beyonce, mara baada ya taarifa zilizotoka toka Hollywood zikimweleza
mwanamuziki huyo kwamba yuko kwenye hatua za maandalizi ya kutengeneza
filamu ya historia ya maisha ya mwanamama Saartjie Baartman, aliyekuwa akitumikishwa kama mtumwa mwenye mvuto ambapo Beyonce ndiye angesimama kama mwanamama huyo.
Kwa kuona hivyo GSENGO BLOG
ikaona ni kheri sasa kukupa japo kwa ufupi historia ya mwanamama huyo
na hata picha zake ili nawe ufanye mlinganisho na mwisho wa siku upate
nafasi ya kukomenti kuhusu hatua hiyo au kama vipi mbelembele ikibidi
uwe na pendekezo lako. (ukiamua)
Sasa ipate kwa njia ya sauti simulizi ya Mwanamke mrembo "Sarah" Baartman
aliyezaliwa miaka ya kabla ya 1790 – 29 December 1815) akifanya kazi
kama mtumwa mjini Cap Town nchini Afrika ya Kusini akiwa na sifa ya kuwa
na umbo la kiafrika lenye taswira ya kuwa na makalio makubwa ambaye
inasadikika kuvunja rekodi kwa wanawake wote waliopata kutokea
ulimwenguni hata wazungu wa utawala wa kikoloni kumchukua hadi nchini
Uingereza na kumtumia kama maonyesho.
Lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 26 tu...na ni kwa ugonjwa wa zinaa.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA Simulizi
ya iliyosimuliwa kupitia kipindi cha majira ya jioni kupitia kituo cha
radio cha Jembe Fm Mwanza ukiwa na Jaqueline Shuma, Timoth Ngalula na
Babu Mkombe