Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said amefariki
dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya kuogelea,taarifa
zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Bwa.Suleiman alikimbizwa hospitali ya
Agakhan kwa matibabu,na baadae ikaelezwa kuwa amekwishafariki na kuwa
mazishi yanatarajiwa kufanyika leo. Marehemu alipata kuwa Katibu mkuu wa
Simba alikopewa jina la Yelstin.Taarifa zaidi tutazidi kufahamishana
kadiri ya zikavyokuwa zikiingia.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.