Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa nje toka
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa Habari leo jijini Dara es salaam
kuhusu utaratibu mpya wa utoaji wa Huduma kwa wagonjwa wa nje ambapo
huduma zitakuwa zikitolewa kuanzia Jumatatu hadi jumamosi ikiwa ni moja ya
mikakati ya Hosipitali hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi
Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi
Neema Mwangomo akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Vyombo vya habari
amabapo aliwataka Watanzania kutumia huduma zinazotolewa na Hospitali hiyo ya
Taifa kwa kuwa inao wataalamu wakutosha
kutimiza jukumu hilo la kuwahudumia wananchi.
Mkuu wa Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa nje toka
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akisisitiza jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano ulioenga kueleza
mikakati ya Hosipitai hiyo katika kuboresha huduma zake kwa wananchi.kushoto ni
Afisa Uhusiano wa Hospitali hiyo Bi Neema Mwangomo na kushoto ni Muuguzi wa
Hospitali hiyo Bi June Samwel.
Hospitali ya Taifa Muhimbili
imesema kuwa inaendelea kuboresha huduma za afya ili kupunguza msongamano wa
wagonjwa kupitia utaratibu mpya wa madaktari
Bingwa kuwaona wagonjwa kupitia Kliniki zilizoanzishwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Idara ya Huduma
ya Wagonjwa wa Nje wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond Mwenesano akizungumza
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo leo jijini Dar es
salaam amesema kuwa utaratibu huo utawasaidia wagonjwa kupata huduma kwa wakati
na kupunguza muda kusubiri huduma.
Amesema utaratibu huo
utawahusu wagonjwa wote wanakwenda kutibiwa katika Hospitali ya Muhimbili na
kuondoka hususan wale wanaolipa fedha taslimu na wale ambao ni wanachama wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bima za mbalimbali za Afya na watumishi ambao
makampuni yao yana mikataba na Hospitali kutibu wafanyakazi wao.
Dkt. Mwenesano ameeleza
kuwa tayari Kliniki hizo zimekwisha anza kufanya kazi na kuongeza kuwa katika
hatua hiyo madaktari Bingwa pekee ndiyo watakaoona wagonjwa wakati wa siku za
kazi kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni, pia jumamosi kuanzia saa 3
asubuhi hadi za 8 mchana.
“ Muhimbili tumeamua
kufanya mabadiliko haya kuanzisha Kliniki na kuwatumia madaktari bingwa peke kwa lengo la kuboresha
huduma zetu, awali tulikuwa na Kliniki hizi lakini huduma zake zilikuwa hazitolewi
kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na kutokuwepo kwa muda wa kutosha wa
mdaktari hao kuhudumia wagonjwa” Amesisitiza.