Jumba la Mchungaji Mama Rwakatale
Wakati operesheni ya kuweka alama ya X
kwenye nyumba zilizojengwa mabondeni, maeneo ya wazi na kinyume na
taratibu ikiendelea, Hoteli za Double Tree na Slip Way nazo zimekumbwa
na pigo hilo.
Hoteli hizo pamoja na nyumba ya
Maheshbhai Patel na baadhi ya wamiliki wengine wa nyumba ambao kuta zake
zimejengwa karibu na barabara ya Slip Way eneo la Msasani Peninsula,
wamepewa siku saba kuzibomoa.
Jumba la Mama Rwakatale likiwa limekewa alama ya X
Jana, uongozi wa Manispaa ya Kinondoni
uliweka alama za X na kuwaonya wamiliki hao kwamba, wasipobomoa
manispaa itazibomoa na kudai gharama za ubomoaji.
Bomoa.
Akizungumza kwa simu jana, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema Serikali
haitaurudi nyuma katika kutekeleza sheria hata kama kuna watu wana jeuri
ya pesa.
Alisema
Manispaa ya Kinondoni iliwapatia vibali vya kupendezesha maeneo ya
pembezoni mwa barabara ikiwamo kupanda maua, lakini wao badala ya
kutimiza masharti ya vibali walizungushia kuta jambo ambalo
hawatalivumilia.
“Wangependezesha na kufunga
minyonyoro kuzuia kuharibiwa mazingira yao kama walihisi wananchi
wangeharibu, lakini siyo kujenga kuta.
“Nimewaagiza Kinondoni wawapatie notisi ya siku saba kubomoa kwa hiari. Wasisubiri Serikali ivunje.
“Tutabomoa hadi lile jengo lililopo karibu na Hospitali ya Ami lililovunja sheria, yule hawezi kuonyesha jeuri ya fedha,” alisema Lukuvi.
Alisema Serikali ina mpango maalumu wa
kubomoa majengo yote yaliyojengwa kinyume na sheria Masaki na Oysterbay
na wameanza na Barabara ya Slip Way.
Katika hatua nyingine, sakata la
bomoabomoa pia limewakumba waliojenga katika hifadhi za mikoko baada ya
watumishi wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na maofisa misitu
wa Manispaa ya Kinondoni kuweka alama ‘X’ katika nyumba zaidi ya 30
ikiwamo ya kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, Dk Getrude Rwakatare.
Kazi hiyo ilianza jana mchana katika
maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam ikiwamo, katika Mtaa wa Ally Sykes,
Kawe na Jangwani Beach eneo la Mbezi Beach. Ofisa Misitu Msaidizi wa
Manispaa ya Kinondoni, Issa Juma aliwaambia wanahabari kuwa kazi hiyo ni
endelevu