Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha
waliojitokeza kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga
zoezi la Onesha uwezo Medani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisoma bango mara baada ya kukabidhiwa na mwananchi mmoja katika eneo
la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha
Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani Arusha.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha
Tech. Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis
Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani
lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis
Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha
Uwezo Medan.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la
Ufungaji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara
baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
katikati akishuhudia matukio ya zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli
Mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akipewa maelezo ya zana mojawapo ya Kivita katika Zoezi la Onesha Uwezo
Medani Mkoani Arusha. Picha na IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunga
“Zoezi la Onesha Uwezo Medani” lililoandaliwa na kutekelezwa na Kamandi
ya Jeshi la Nchi Kavu ambalo ni sehemu ya Jeshi la wananchi Tanzania
katika eneo la Lang’arurusu nje kidogo ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi
Monduli Mkoani Arusha.
Akizungumza
na Askari na Maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania kabla ya kufunga
zoezi hilo, Rais Magufuli amesema katika awamu yake ya tano ya uongozi
amedhamiria kulitumia Jeshi la wananchi Tanzania katika kujenga uchumi,
ikiwemo kuanzisha viwanda na kampuni za ujenzi ili kuharakisha
maendeleo.
Ametoa
mfano wa kiwanda cha Nyumbu ambacho kipo chini ya jeshi la wananchi
Tanzania na kueleza kuwa wakati umefika wa kukiimarisha na kukiendeleza
kiwanda hicho, ili kiweze kufanya uzalishaji mkubwa kwa manufaa ya nchi
ikilinganishwa na hali ilivyo hivi sasa.
“Zipo
nchi nyingi ambazo majeshi yao yanatumika katika uchumi na yanafanya
kazi nzuri ya kupigiwa mfano, wakati umefika na sisi kufanya hivyo. Hata
hizi sare za jeshi na viatu, hatuna sababu ya kuvinunua kutoka nje ya
nchi, tunaweza kutengeneza sisi wenyewe” Alisisitiza Rais Magufuli.
Rais
Magufuli amelipongeza Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuandaa
“Zoezi Onesha Uwezo Medani” ambalo limethibitisha uwezo, weledi na
utayari lilionao katika jukumu lake la kiulinzi.
Ameahidi
kuwa ataendeleza juhudi zilizofanywa na viongozi wenzake waliotangulia
za kuliimarisha kwa vitendea kazi na maslai ya wanajeshi ili liweze
kutekeleza wajibu wake bila vikwazo.
Pamoja
na kuwapongeza Askari na maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania
walioshiriki katika zoezi hilo, Rais Magufuli ameagiza Askari Mgambo na
Askari wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) walioshiriki zoezi hilo kuajiriwa
na jeshi la wananchi Tanzania.
Akitoa
maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Rais Magufuli, Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Wizara yake
itaongeza na kusimamia juhudi za kuliboresha jeshi hilo kwa zana, vifaa
na maslai kwa wanajeshi ili kuwajengea uwezo na morali ya kutekeleza
majukumu yao ya kuilinda nchi, pamoja na kutoa msaada stahiki kwa nchi
zenye kuhitaji ulinzi wa amani popote duniani.
Kwa
upande wake Mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Adolf
Mwamunyange amemhakikishia Rais Magufuli kuwa Jeshi la wananchi Tanzania
lipo imara na litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, nidhamu
ya hali ya juu na uzalendo mkubwa.
Kabla
ya kuwahutubia maafisa wa jeshi la wananchi, Askari na wananchi
waliohudhuria ufungaji wa “Zoezi Onesha Uwezo Medani”, Rais Magufuli
ameoneshwa zana mbalimbali za kivita ikiwa ni pamoja na kushuhudia
upigaji wa mizinga ya masafa mafupi, masafa ya kati na masafa marefu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
22 Januari, 2016