Rick Ross “Rozay” (katikati) na Mkurugenzi wa Epic Records, L.A. Reid (kushoto) pamoja na msaidizi wake Sylvia Rhon.
Los Angeles, Marekani
HABARI njema ikufikie: Staa wa muziki
nchini Marekni, Rick Ross “Rozay” ameendelea kujipanua kikazi mwaka huu
mpya wa 2016. Rozay ameamua kuachana na kampuni ya muziki aliyokuwa
akifanya nayo kazi tangu mwaka 2006 ya Def Jam na kupata dili nono kwenye kampuni ya Epic Records.
Picha za Rozay alizoweka kwenye akaunti
yake ya twitter wikiendi iliyopita zilimuonesha yeye na Mkurugenzi wa
Epic Records, L.A. Reid pamoja na msaidizi wake Sylvia Rhon huku Rozay
akiandika: “Welcome @rickyrozay to the #EPIC family!”
Rozay alisaini mkataba na kampuni ya Def
Jam mwaka 2006 na kufanya albamu nane kwenye lebo hiyo ya Epic kuanzia
kipindi hicho mpaka anapoondoka kwenye kampuni hiyo. Albamu yake ya
mwisho kufanya na Def Jam ni ile aliyoiachia Decembere mwaka jana ya Black Market, ambayo inatamba na kushika namba 6.
Rozay amejiunga na wasanii kibao walioko
kwenye lebo ya Epic wakiwemo; Future, Diddy, Mariah Carey, Ciara,
Travis Scott na Fifth Harmony.
Ross pia anadili jingine na Warner Music
kwa ajili ya Maybach Music Group yenye wasanii wakali kama Meek Mill,
Wale, Stalley, Rockie Fresh na Omarion. MMG pia anahusishwa kuhamia Epic
Muda wowote.