Meneja Mkuu wa Tigo, Deigo Gutierrez
Na mwandishi Wetu
KAMPUNI ya MIC Tanzania Limited (Tigo) chini ya mkurugenzi wake, Diego Gutierrez imepigwa faini ya Sh. Milioni 25 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kosa la kushindwa kudhibiti utumaji wa ujumbe wa ulaghai na udanganyifu kwa wateja wake.
KAMPUNI ya MIC Tanzania Limited (Tigo) chini ya mkurugenzi wake, Diego Gutierrez imepigwa faini ya Sh. Milioni 25 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kosa la kushindwa kudhibiti utumaji wa ujumbe wa ulaghai na udanganyifu kwa wateja wake.
Taarifa ya faini hiyo ilitolewa hivi
karibuni jijini Dar na Mkurugenzi wa TCRA, Dk. Ally Simba ambapo alisema
kampuni hiyo na makampuni mengine ya simu, yameshindwa kudhibiti
utumaji wa ujumbe wa udanganyifu na kuwalaghai wateja.
Taarifa hiyo ilizidi kueleza kuwa, Tigo
inapaswa kulipa faini ya Sh. Milioni 25 ambapo amri hiyo imetolewa hadi
Januari 29, 2016 na endapo hawatafanya hivyo, mamlaka hiyo itachukua
hatua za kisheria na kuidhibiti kampuni hiyo.
Mbali na ulaghai huo wa kupitia ujumbe
mfupi wa maneno (SMS), Novemba 8, mwaka huu Tigo ililalamikiwa na wateja
wake kwa kutokuwa hewani siku nzima kitu ambacho kiliwasababishia
wateja hao kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo kwa kukosa
mawasiliano.
“Hawa Tigo hawapo makini kabisa.
Haiwezekani kwa watu makini mtandao ukosekane siku nzima,” alilalamika
mmoja wa watumiaji wa mtandao huo.
Mbali na hilo, watumiaji mbalimbali wa
mtandao huo wamekuwa wakiulalamikia kwa kutoa huduma hafifu licha ya
kujitangaza kuwa wapo vizuri.
“Kuna wakati wewe wa Tigo unampigia wa
Tigo mwenzako, hapatikani! Ukirudia unampata na anakwambia hajazima
simu. Huu ni uzembe mwingine wa mtandao. Lakini pia inaweza kuleta balaa
zaidi ya wanavyofikiria wao Tigo,” alisema John, mkazi wa Dar.
Mbali na Tigo, makampuni mengine
yaliyopigwa faini kwa kosa la kushindwa kudhibiti ujumbe wa udanganyifu
na ulaghai kwa wateja ni pamoja na Benson Informatics Limited (Smart),
Airtel Tanzania Limited Viettel Tanzania Limited (Halotel) na Zanzibar
Telecom Limited (Zantel).