Mataili yaliyochomwa barabarani wakati wa taflani hiyo. Hali ilivyokuwa eneo la tukio. Gari la ‘washawasha’ likiwa eneo la tukio.
Kikosi cha FFU wakiimarisha ulinzi. Polisi wakiimarisha ulinzi eneo la tukio.…Wakijadiliana jambo.
WAKAZI wa eneo la Bonde la Mkwajuni,
Kinondoni jijini Dar es salaam leo wamefunga Barabara ya Kawawa kwa muda
wakipinga ‘Bomoabomoa’ ya nyumba zao.
Katika kuonyesha hasira zao, wakazi hao
wamechoma matairi na kujaza magogo barabarani na kupelekea usumbufu kwa
watumiaji wa barabara hiyo.
Baadaye Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kukabiliana na vurugu hizo.
(Picha: Denis Mtima/Gpl