Afisa
Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini
Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha
shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika
ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Afisa
Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini
Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla
moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua
zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
Mmoja
wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama
(ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama
alivyokutwa na mpiga picha wetu.
Na Modewjiblog, Team.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa
kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo
watamchukulia hatua kali.
Kauli
hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla
alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo
jijini Dares Salaam.
Dk.
Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama
mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo
kufukuzwa kazi.“Kwa
watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama
itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!.
Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu
wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja
na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.