Mamia ya wafuasi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama
hicho, Freeman Mbowe leo wamefurika kwenye eneo la Mahakama Kuu Kanda
ya Mwanza katika kesi ya mbunge wa zamani wa Nyamagana, Ezekiel Wenje
(CHADEMA) anayepinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka
jana yaliyompa ushindi wa ubunge wa jimbo hilo, Stanslaus Mabula (CCM).
Polisi wametumia nguvu ya ziada kuhakikisha ulinzi unaimarika mahakamani hapo.