Inafika Band au Wazee wa Indege.
INAFRIKA BAND IMETEULIWA KUIWAKILISHA AFRIKA NCHINI MAREKANI
Katika maonyesho makunbwa ya Festival Of Nations,katika Dollywood Theme Park.
Bendi maarufu Inafrika band aka Wazee wa
Indege wanatarajiwa kuruka wakati wowote ule kuelekea nchini marekani
kushiriki katika maoyesho makubwa ya kimataifa ya Festival of nations
,yatakayo fanyika katika Dollywood Theme Park,bendi hii kutoka Tanzania
ndio bendi pekee iliyoteuliwa kuliwakilisha bara la Afrika katika
maonyesho hayo ya kimataifa.
Inafrika
band itakuwepo nchini marekani katika ziara ya kikazi kwa muda wa miezi
mitatu kuzikonga nyoyo za washabiki wa kimataifa nchini
marekani. Kuchaguliwa kwa Inafrika band kushiriki maonyesho hayo makubwa
kunatokana na mvuto wa muziki wa bendi hiyo kukubalika zaidi kimataifa.
Muziki
ambao una maadili ya kitanzania ambako nje ya mipaka
umewateka washabiki wengi wa kimataifa. Bendi hiyo yenye makao jiji
Dar-es-salaam imejikuta haina muda wa kupumzika kutoka na wingi Tour za
kimataifa kwa muda wa miaka 10 sasa.
Ni
kama wiki mbili tu bendi hiyo imerudi kutoka safari ya nchi 19 za bara
la ulaya. Tunawatakia kila la heri Inafrika Band aka Wazee wa Indege
katika kutuwakilisha huko Marekani. Bendi hiyo ilikuwapo Dollywood
,Marekani mwaka 2014 na kuwanasa washabiki wengi na muziki wao wa
kitanzania
Watupie jicho at http://www.inafrikaband.co.tz au
http://www.facebook.com/inafrikaband.wazeewaindege
http://www.facebook.com/inafrikaband.wazeewaindege