Mwenyekiti
wa Chama cha CHADEMA Taifa,Mh.Freeman Mbowe
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha shughuli zote za
maandamano na mikutano nchi nzima,kwa kudai kuwa ukuta ni fikra endelevu na si mpango
wa siku moja.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti
wa Chama hicho Taifa,Mh.Freeman Mbowe wakati akizungumza
na Waandishi wa Habari,Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Mbowe amesema kuwa wataendelea Kujipanga katika kulinda Haki yao ya kidemokrasia kama ambavyo katiba
ya vyama vya siasa inavyosema,kuwa ni haki yao ya kidemokrasia.
‘’Mapambano ya kisiasa si tukio la siku moja ni tukio
endelevu na kwa hiyo tarehi Mossi ,Oktoba ambayo ilikuwa ni siku mbadala ya maandamano
maalum,hivyo kwa niaba ya kamati kuu imeona kuna umuhimu wa kusimamisha maandamano maalumu na mikutano
nchi nzima ilikupisha mbinu nyingine mbalimbali’’amesema Mbowe
chanzo,Globu ya Jamii