Dr.Charles John Tizeba-Waziri mpya Wa Kilimo,Uvuvi na Mifugo
Waziri mpya Wa Kilimo,Uvuvi na Mifugo Dr.Charles John Tizeba leo tarehe30/09/2016 amekutana na kufanya kikao na wadau wa sekta ya kilimo cha pamba kwa mikoa ya kanda ya ziwa kikao hicho kilichodumu kwa muda wa masaa 5 kiliwakutanisha wadau wa kusambaza mbegu za pamba pamoja na wadau wa uzalishaji mbegu na usamabazaji wa dawa viatilifu.
Aidha Dr.Charles John Tizeba amewataka wadau pamoja na bodi ya pamba kushirikiana kwa pamoja kuweza kuwasaidia wakulima katika zao la pamba ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu juu ya kilimo bora cha pamba kwani kwa sasa kilimo cha pamba kinaonekana kushuka kwa kasi kulinganisha na miaka ya nyuma kidogo ambapo zao hilo lilikuwa na kipaumbele zaidi katika uzalishaji. Hata hivyo Dr.Charles John Tizeba amezitaka mamlaka husika zinazo husika na usambazaji wa mbegu kwa wakulima wa pamba kuhakikisha wanapeleka mbegu zilizo bora ilikuweza kusaidia zao hilo kuwa na soko zuri kwani kumekuwa na baadhi ya malalamiko mengi kwa wakulima wakidai kuwa wasambazaji wa mbegu za pamba wamekuwa wakiwapa mbegu zilizooza na hatimaye wakati wa msimu wa pamba mbegu hizo hazioti kabisa au kupeleka zao hilo kuwa na uvunaji hafifu.
lakin kwa upand mwingine pia waziri wa kilomo uvuvi na mifugo Dr.Charles John Tizeba amewataka wadau wa manunuzi kuweza kupandisha bei kidogo kwa wakulima wa pamba na pia kushusha bei za dawa na mbegu pia amwewataka bodi kusimamia vizuri kazi hiyo na kuhakikisha zao la pamba linakuwa katika mfumo mzuri.
Mhe Waziri Dr.Charles John Tizeba amesema Serikali marekebisho makubwa ndani ya tume ya maendeleo ya ushirika iliyochini ya wizara ya kilimo na uvuvi na kuchukua hatua za kinidhamu kwa watakao husika na ubadhilifu wa mali za ushirika aidha baadhi ya maafisa ushirika waliokaa ktika kituo kimoja kwa muda mrefu watahamishiwa katika maeneo mengine.
TAAFIRA YA WAZIRI WA KILIMO UVUVI NA MIFUGO