Askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond
Tutu amesema katika ujumbe wake wa siku yake ya kuzaliwa katika gazeti
la Washington Post kwamba angependelea kusaidiwa kufa.
Katika
ujumbe huo Tutu alisema: Nimejiandaa kufa na nimesema wazi singependelea
kuendelea kuishi kwa gharama yoyote.Ningependa kutibiwa na mapenzi na
kuruhusiwa kufariki vile nipendevyo.Watu wanaokufa wanapaswa kuwa na
haki ya kuchagua vile na lini watakavyokufa.Ninaamini kwamba,mbali na
uuguzi uliopo ,chaguo lao linafaa kushirikisha kusaidiwa kufa kwa
heshima.Alitangaza hatua yake ya kuunga mkono wazo hilo baada ya kulipinga 2014.
Habari kwamba Desmond Tutu angependa asaidiwe kufa sio swala la kushangaza nchini Afrika Kusini.
Swala la kusaidiwa kufa limeigawanya nchi hiyo kwa kipindi cha muda sasa.
Mwaka uliopita mahakama kuu katika mji mkuu wa Pretoria iliamuru kwa kumpendelea mgonjwa mmoja aliyekuwa anaugua saratani kupitia kiasi, Robin Strasham-Ford ambaye alikuwa ametoa ombi la kusaidiwa kufa.
Alikuwa amesalia na wiki mbili pekee kufariki na alitaka sheria irekebishwe ili asaidiwe kufa bila ya kuwepo kwa kesi.
Sheria ilikuwa wazi,daktari yoyote ambaye angemsaidia mgonjwa kufariki angepewa hukumu ya miaka 14 jela.
Taifa hilo halina sheria ya kusaidiwa kufa,huku katiba ikilinda haki ya kila mmoja ya kuishi.
chanzo bbc