Kila tarehe 15
Oktoba, Dunia nzima huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umasikini,
ambapo mwaka huu kauli mbiu ya siku hiyo ilikuwa ni
‘’KUTOKA
UDHALILISHAJI NA UTENGWAJI MPAKA USHIRIKISHWAJI ‘’.
Mtandao wa Dini
mbalimbali kwaajili ya watoto ulimwenguni uitwao Global Network of Religion for Children
(GNRC-Tanzania) wamefanikiwa kuhitimisha siku hii kwa namna ya pekee kabisa
ambapo tangu tarehe 15 Oktoba wamekuwa wakiandaa matukio mbalimbali yaliyolenga
kuwajengea uwezo watoto haswa wa Shule za msingi kwa kuandaa mashindano tofautitofauti
kama Midahalo na Michezo ikiwa na lengo la
kuwajengea watoto uwezo (capacity building) na kuwapa elimu ambayo itaweza kuwakomboa
katika janga la umasikini .
Washiriki wa
Mdahalo wakisalimiana na Mama Joyce Mdachi kutoka GNRC na viongozi wengine wa
shule
5.Mfano wa vyeti
walivyotunukiwa wanafunzi kutoka na ushiriki mzuri wa siku hii ya kipekee
Vainess
Mbaga (Education Officer) akitoa elimu
kwa watoto
Wanafunzi wa shule ya Msingi Oysterbay wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baraka Chedego kutoka GNRC -Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu
wanafunzi
wakiwa katika mdahalo