Gavana wa jimbo la Florida nchini
Marekani, Rick Scott ameonya kuwa uharibifu utakaotokea utakuwa mkubwa
sana ikiwa kimbunga Matthew kitapiga jimbo hilo.
Bw Scott ametoa
wito kwa wakazi wa jimbo hilo kujiandaa kuhama makwao zoezi ambalo ndilo
litakalokuwa kubwa zaidi katika historia ya jimbo hilo.Msongamano mkubwa wa magari na watu umetokea katika barabara huku watu wakihamia maeneo ya bara.
Wakazi katika jimbo la Carolina Kusini pia wametakiwa kuhama maeneo yaliyo hatarini. Gavana Nikki Haley amesema watu 250,000 watahamishwa kutoka maeneo ya pwani.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kimbunga hicho kinaweza kuwa hatari sana na kuwataka wakazi wa eneo hilo kufuata ushauri unaotolewa na mamlaka
Shule zimefungwa na wagonjwa wametolewa katika baadhi ya hospitali.
Kimbunga kikubwa cha mwisho kukumba jimbo la Florida kilikuwa ni Katrina miaka 10 iliyopita.
Kimbunga Matthew tayari kimepiga mataifa ya Haiti na Cuba.
Watu kumi wamethibitishwa kufariki nchini Haiti lakini hali halisi ya uharibifu na maafa yaliyotokea badi haijajulikana. Watu wanne wamefariki katika Jamhuri ya Dominika.