Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula
na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla, akiwapatia maelezo warembo
hao walipotembelea duka la kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya warembo wa Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula
na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), nje ya duka la The Farm Fresh Market, Victoria jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tomoni, wauzaji wa mbogamboga za majani, nyama, vyakula na juisi za matunda halisi, Franklin Bagalla (katikati), akiwapatia maelezo warembo hao, wakati akiwambeza kwenye sehemu mbalimbali za kampuni hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya warembo wa Miss Tanzania wakiangalia Menu walipofika Mgahawa wa
Kampuni ya Tomoni Farms, Victoria jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya washiriki wa Shindano la Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kuwasili Hoteli ya Regency Msasani jijini Dar es Salaam
leo kuanza kambi rasmi.(Picha zote na Kassim
Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi
wa Lino Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundega
akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo mara baada ya idadi
kubwa ya warembo hao kuwasili tayari kuanza kambi rasmi. Kushoto ni Mkuu
wa Itifaki Albert Makoye na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Miss Tanzania,
Deo Captain.
Warembo
wakiwasili kwenye Duka na Mgahawa wa Kampuni ya Tomoni Farm, la 'The
Farm Fresh Market', maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam kujionea
shughuli mbalimbali zifanywazo na kampuni hiyo, pia kujipatia chakula
cha mchana.
JUMLA
ya washiriki 30 wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania wameanza kambi
ya mwezi mmoja leo tarehe 30 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam.
Washiriki
hao ambao ni washindi kutoka Kanda 9 na mikoa mbalimbali Tanzania
watapokelewa katika Hotel ya Regency Park iliyopo Mikocheni D’salaam, na
baadae watapiga kambi ya siku 4 katika Hotel ya Jozi Lounge iliyopo
Msasani jijini D’salaam.
Mara
baada ya kuingia kambini washiriki hao 30 pamoja na Wasimamizi wao
watakuwa na Semina ya pamoja ambapo watafundishwa masuala mbalimbali
yahusuyo mashindano pamoja na kambi kwa ujumla.
Wakiwa
kambini washiriki hao watafanya ziara katika mikoa ya Dodoma, Singida,
Arusha, Geita na Mwanza kwa shughuli mbalimbali za kijamii.
Kauli
mbiu ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 ni Urembo na Mazingira Safi,
hivyo washiriki wote watafanya kazi mbalimbali kijamii ikiwa ni pamoja
na usafi wa mazingira, kutunza mazingira na pia kushiriki katika
kampeni ya kupanda miti itakayofanyika tarehe 1 Oktoba 2016 nchini pote.
Mashindano
ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 yamekuwa na changamoto kubwa
ya kupata wadhamini wachache waliojitokeza kudhamini mashindano haya
katika mikoa na sehemu mbalimbali.
Tunachukua
fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Wadhamini wote waliojitokeza na
kuchangia kwa njia mbalimbali katika kufanikisha mashindano ya mwaka
huu.
Tunawashukuru
pia washiriki wote katika ngazi zote waliojitokeza kushiriki na pia
shukrani kwa wazazi na walezi walioruhusu watoto wao kushiriki
mashindano ya urembo ya miss Tanzania 2016.
Ni
matarajio yetu kwamba wadau wote wa tasnia hii ya urembo nchini
mtajitokeza kwa wingi katika Fainali za Shindano la Miss Tanzania 2016
linalo tarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2016.
ORODHA YA WAREMBO WA MISS TANZANIA 2016
JINA
|
MKOA/ KITUO
|
KANDA
|
|
DAR CITY CENTRE
UKONGA
TABATA
DAR CITY CENTRE
|
KANDA YA ILALA
|
|
UBUNGO
DAR INDIAN OCEAN
SINZA
SINZA
|
KANDA YA KINONDONI
|
|
LINDI
MOROGORO
MOROGORO
MTWARA
|
KANDA YA MASHARIKI
|
|
DODOMA
SINGIDA
SINGIDA
|
KANDA YA KATI
|
|
IRINGA UNIVERSITY
|
KANDA YA ELIMU YA JUU
|
|
GEITA
MWANZA
GEITA
|
KANDA YA ZIWA
|
|
ARUSHA
KILIMANJARO
TANGA
MANYARA
|
KANDA YA KASKAZINI
|
|
IRINGA
IRINGA
RUVUMA
MBEYA
|
KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
|
.
|
MBAGALA
KIGAMBONI
MBAGALA
|
KANDA YA TEMEKE
|