Basi hilo lenye
namba T 101 CUU lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kijiji cha
Mahuta katika Wilaya ya Newala Mkoani Lindi, lilipinduka baada ya gurudumu lake
la kushoto kupasuka na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo na mwingine 1
kufariki dunia baadaye akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya
Lindi, huku watu wengine 43 wakiwa wamejeruhiwa.
Katika salamu
zake, Rais Magufuli amesema amepokea taarifa za vifo vya watu hao kwa mshituko
na huzuni kwa kuwa kwa mara nyingine Taifa limepoteza watu wake na familia
zimepoteza wapendwa wao na watu ambao ziliwapenda na kuwategemea.
"Ndugu Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi naomba unifikishie salamu nyingi za pole kwa
wote waliopoteza jamaa na ndugu zao katika ajali hii, kwa hakika nimeguswa sana
na vifo hivi na naungana na familia za marehemu wote katika maombolezo na sala"
amesema
Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli
amewasihi wote walioguswa na vifo hivyo kuwa na moyo wa subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi na amewaombea Marehemu wote
wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Pia Rais Magufuli
amewaombea majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kurejea
katika shughuli za ujenzi wa Taifa,
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
18 Oktoba,
2016