MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Oct 13, 2016

TAKUKURU MWANZA WAMUNSA ALIYEJIFANYA AFISA WA JESHI LA WANANCHI JWTZ KWA UTAPELI WA FEDHA

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Bw. Erest Makale akitoa taarifa hii leo katika ofisi zake. 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mwanza, imemkamata Bi. Felister Mathias kwa kosa la kujifanya Afisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kujipatia pesa Tshs. 240,00/= badaya ya shilingi laki tano (500,000/=) alizoomba kutoka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ernest Makale anasema kuwa Bi. Felister Mathias Mawe aliomba shilingi 500,000/= kutoka kwa mwananchi huyo ili aweze kumsaidia kupata nafasi ya kujiunga na jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) BOFYA KUSIKIA TAARIFA HIYO.
Mtuhumiwa Bi. Felister Mathias Mawe akisimulia waandishi wa habari kilichotokea mpaka akaingia kwenye mtego huo wa kutapeli. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

Mtuhumiwa Bi. Felister Mathias Mawe
Mwanajeshi Mstaafu Bi. Sophia Chacha.
Aidha Mwanajeshi Mstaafu Bi. Sophia Chacha naye amekamatwa na kuhojiwa akitajwa kuwa amekuwa akimsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na jeshi hilo hasa wasichana. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA AKISIMULIA ANAMFAHAMU VIPI MTUHUMIWA.

Bi. Felister alikamatwa na TAKUKURU mnamo tarehe 10/10/2016 katika Hoteli ya Wendele iliyopo Kirumba jijini Mwanza.

Mtuhumiwa tajwa amekuwa akijipatia fedha kwa watu mbalimbali waliokuwa wakihitaji kujiunga na jeshi hilo kwa madai kwamba atawasaidia kupta nafasi kwa kiwango cha shilingi laki tano (500,000/=) kwa kil mmoja.

Aidha kwa mujibu wa ushahidi uliopatikana kitendo cha mtuhumiwa kujifanya Afisa wa Jeshi hakihusiani na Makosa yaliyo chini ya sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11/2007, hivyo jalada lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa Wakili wa Seriali Mfawidhi ili Mtuhumiwa aweze kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.