Kenya imewasilisha jina la waziri
wake wa maswala ya kigeni Amina Mohamed kuwania wadhfa wa uenyekiti wa
tume ya umoja wa Afrika AU.
Mwenyekiti wa sasa Nkosazana Dlamini
Zuma ambaye alitarajiwa kujiuzulu mnamo mwezi Julai wakati wa kikao cha
umoja huo mjini Kigali Rwanda,aliamua kusalia uongozini hadi kikao
chengine baada ya wagombea watatu waliokuwa wakigombea wadhfa huo
kushindwa kupata thuluthi mbili za wingi wa kura.