Katika Mwaka mmoja wa Rais Magufuli, mikakati imeshawekwa kwa ajili ya kujenga upya Reli ya Kati na Bomba la Mafuta kutoka Uganda. Miradi hii ikikamilika hakika Tanzania tutakuwa tunapata fedha nyingi za kigeni na hivyo kuweza kugharamia mahitaji mengi ya ndani.
Rais Magufuli pia kawaalika majirani zetu wa Rwanda, Zambia, Uganda, DRC na kaalikwa Kenya kwa lengo la kuhakikisha Wanafanya biashara na Tanzania na hivyo kutengeneza fedha lukuki.
Rais wetu pia kafanya mambo makubwa katika kubana matumizi yasiyo ya lazima. Nadiriki kusema kuwa Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli umetosha kumzika Lowasa kisiasa na sijui hata akigombea tena 2020 atakuja na sera zipi.
By Lizaboni/Jamii Forums