Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiteta jambo na mkewe Neema baada ya mahakama kumalizika
Na.Vero Ignatus,Arusha
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Dkt.Modesta Opiyo amewapa siku
kumi(10)mawakili wa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wawe
wamewasilisha notisi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya
chini iliyomnyima dhamana Lema .
Agizo
hilo limekuja kutokana na Mahaka kutoridhishwa na hoja za maombi ya
mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya taarifa
ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa Mbunge huyo.
Jaji
Dkt.Modesta Opiyo wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alisema katika
maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta
maombi walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya
kuitwa mahakamani,ambapo amesema mahakama haijaona ucheleweshwaji wa
lazima.
Baada
ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shekh Mfinanga na
Faraji Mangula kuwasilisha notisi ndani ya siku kumi kuanzia leo,hadi
hapo tar 30dec2016 shauri hilo litakaposikilizwa tena.
****TUJIKUMBUSHE****
Mbunge
Godbless Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika
mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha
Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya
kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.
Mbunge
huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa
kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata
mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa
kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi
waliomchagua kuwa Rais wa nchi.