MADIWANI
wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wakiendelea na vikao vya kamati ,ambapo
wamewasimamisha kazi watumishi wawili,ili kupisha uchunguzi wa upotevu
wa takribani milioni 42 pamoja na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya
maendeleo kiasi cha shilingi milioni 250.
Na Rhoda Ezekiel -Globu ya Jamii Kigoma,
MADIWANI
wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia vikao vya kamati wamewasimamisha
kazi watumishi wawili,ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa takribani
milioni 42 pamoja na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo
kiasi cha shilingi milioni 250.
Maamuzi
hayo yalichukuliwa mara baada ya kamati mbalimbali kujiridhisha na
upotevu wa fedha kiasi cha milioni 42 ambazo zilihamishwa kutoka akaunti
ya Amana na kupelekwa kwenye akaunti ya maendeleo na kutumiwa kulipa
miradi mingine ya maendeleo iliyokuwa ikisimamiwa na Manispaa hiyo
lakini pia matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 250
ambapo tume imeundwa ili kuchunguza zaidi tuhuma hizo.
Akitoa
ufafanuzi Meya wa Manispaa hiyo Hussen Ruhava,mara baada ya maamuzi
hayo alisema tume imeundwa kuchunguza watumishi wanne kati ya sita
wamechukuliwa hatua za kinidhamu na kuwajibika kulipa fedha hizo huku
kati ya hao wawili wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi na hatua za
kisheria zitachukuliwa.
Ruhava
aliiwataja walio simamishwa kuwa ni Christina Nayingu ambae ni Mhasibu
wa Manispaa na Michael muhadhini wa Ndoliwa Muhadhina wasultani
Ndoliwa na Dr Johni Tratra kuwa watasimamishwa ili kupisha uchunguzi
pindi utakapo kamilika,na watatakiwa kulipa kiasi chote cha fedha
kilicho tolewa.
Aidha
Ruhava alisema licha ya maamuzi hayo lakini pia wameeleza kutokuwa na
imani na Mkurugenzi wa Manispaa Judethadeus Mboya kutokana na kushindwa
kukusanya mapato ipasavyo, asilimia kumi kutotolewa kwa vijana na
wanawake, sanjari na asilimia 20 ya maendeleo kutokufika katika maeneo
husika lakini pia sakata hilo lilimkumba na afisa mipango miji kushindwa
kutekeleza maamuzi ya vikao vya madiwani na hivyo kuchukuliwa hatua za
kinidhamu.
"
hatutaki kufanya maamuzi ya kumuonea mtu, hatutaki kuchukua maamuzi ya
kuwa karibisha watu, tunacho hitaji watumishi wafanye kazi ya
kuwatumikia wananchi bila ubadhilifu wowote na kutenda haki ",alisema
Ruhava
CHANZO MICHUZI MEDIA