MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Feb 24, 2017

TCRA Yaadhibu Vituo Vinne vya Utangazaji

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  imetoa adhabu kali kwa vituo vinne vya utangazaji  kwa kukiuka maadili ya utangazaji kwa mujibu wa sheria na kuvitaka viombe radhi siku tatu mfululizo kuanzia leo (Ijumaa) kupitia taarifa ya habari.

Akitoa adhabu hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka amesema vitio hivyo vimepewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kuomba radhi wasikilizaji wake.

Amevitaja vituo  hivyo kuwa ni Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM.