Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya Serengeti
Boys kueleka kwnye kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17
yatakayofanyika nchini Gabon. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari katika
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas na
Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano
Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal
akiwa pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge
wakiwasikilizisha waandishi ala za wimbo unaotarajiwa kutumika kwa ajili
ya kuhamasisha kuichangia Serengeti Boys
KUELEKEA fainali ya kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya
miaka 17 nchini Gabon, kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys inayoongozwa
na Mwenyekiti Charles Hilal imeandaa wimbo wa pamoja utakaoimbwa na
wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseebb Abdul ‘Diamond’ na
Ali Saleh ‘King Kiba' pamoja na wasanii wengine.
Wimbo huo wa pamoja ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha kampeni za
kuchangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti
Boys itakayofanyika mwezi wa tano nchini Gabon ambapo zitapatikana nchi
nne zitakazokwenda kombe dunia la vijana nchini India.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Charles Hilal amesema kuwa kwa pamoja
wimbo utakaowahusisha wasanii wengine mbalimbali utakuwa na lengo kuu la
kuhamasisha wananchi, wadau na wapenda michezo kuichangia timu hiyo ya
vijana kwa lengo la kuisaidia malengo waliyokuwa wameyafikia ya
kuipeleka timu hiyo kwenye fainali za kombe la Dunia nchini India.
Hilal amesema kuwa hatua hii ya kusaidia Serengeti Boys
kutawajenga vijana hawa kufanya vizuri katika michuano ya mataifa Afrika
kwa vijana ikiw ani pamoja na kupata kambi nje ya nchi na kuchgeza
mechi kadhaa za kirafiki kutoka nchini jirani lakini hata hivyo bado
wanafikria kutafuta mechi ya kirafiki itakayochezwa hapa hapa Jijini Dar
es salaam ikiwa ni kwa ajili ya kuwaaga kuelekea nchini Gabon.
Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge amesema kwamba
tayari ala za wimbo huo zimekwishatengenezwa na wasanii hao wote
wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti, ili mara moja wimbo huo
ukamilishwe na kuanza rasmi kusaidia kampeni ya kuhamasisha Serengeti
Boys.
“Tayari wasanii Ali kiba na Diamond wameshakubali kurekodi nyimo
hiyona wameahidi kufanya haraka kuingiza sauti kwenye ala ambazo
tumeshawatumia na baadae wasanii wengine kama Mwasiti Almasi, Darasa na
Vanesa Mdee nao wataweka sauti zao,"amesema Kitenge.
Kiba na Diamond wote wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na
kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia Serengeti Boys
iliyofuzu Fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.
Katibu wa Kamati hiyo ni Mwesigwa Selestine ambaye pia ni Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Kitenge wa
EFM Radio na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania,
Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu, yumo
Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric
Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.
Pia, Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa kila hatua
kuanzia Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya Hamasa
kwa lengo la kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.