Mzee Yusuf
Aliyekuwa mmiliki wa band ya
Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf amefunguka na kusema toka ameamua
kuachana na biashara ya muziki na kumrudia Mungu maisha yake yameyumba
sana lakini amekuwa na amani, furaha na maisha hayo kuliko kipindi cha
nyuma.
Mzee
Yusuf amesema wakati anafanyakazi ya muziki alikuwa na maisha bora sana
na kufanya vitu ambavyo anataka kufanya bila wasiwasi wowote tofauti na
sasa ambapo akihitaji kitu fulani lazima ajipange kweli kweli ili
kukipata.
"Maisha niliyonayo sasa ni
maisha ambayo yana amani kuliko maisha niliyokuwa nayo huko nyuma, haya
ni maisha ya utulivu kwa hilo nashukuru Mungu, lakini si yale maisha
bora kama niliyokuwa nayo kipindi kile naweza kutaka pilau leo, biliani
kesho napika lakini leo hii nikitaka biliani lazima nijipange, kwa hiyo
uchumi kwangu umeyumba sana lakini nashukuru sina wasiwasi, yaani sina
pressure katika maisha yangu" - alisisitiza Mzee Yusuf.