STAA wa filamu Bongo Jacqueline Wolper amesema kuwa, japo wanaume wengi
wenye nazo wamekuwa wakimsumbua kumtaka kimapenzi, haoni haja ya kuwa
nao kwa kuwa anaamini ni wasumbufu tu hawana mapenzi ya kweli.
Akizungumza mawili-matatu na Star Mix, Wolper alisema, kutokana na
upendo wa kweli anaojitahidi kumuonyesha mwanaume anapokuwanaye kwenye
uhusiano na kujikuta akiambulia maumivu, ameona bora aweke kando masuala
ya mapenzi na kuwa`bize’ na kazi zake. “Sina mpenzi kwa sasa nimeona
bora niweke pembeni haya mambo nidili na kazi zangu tu ndo muhimu,
nikipenda hawa wanaonisumbua `now’ nitapenda na nitakuwa kimapenzi,
lakini bado wote wanaonisumbua hakuna aliyefaulu kunishawishi niwe
naye,” alisema Wolper