Akizungumza leo katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Diamond Platnumz amemwagia sifa mrembo huyo na kusema kuwa amekuwa msaada mkubwa sana kwake hata wakati anaandaa manukato yake ya Chibu (Chibu Perfume).
“Mimi na Wema Sepetu huwa tunawasiliana kwenye simu, na mara kadhaa hukutana sehemu ambazo hazina watu wengi, kwa sasa tumekua. Kila mmoja wetu kwa sasa anajikita kwenye uhusiano wake. Wema Sepetu ana familia yake, lakini uhusiano wetu umejikita katika kusaidiana kibiashara.”
Diamond Platnumz aliongeza kuwa, Wema Sepetu ndiye aliyemshauri kutumia maneno “The Scent You Deserve” kwenye manukato yake aliyoyatambulisha hivi karibuni.
Diamond Platnumz na Wema Sepetu walikuwa ni ‘couple’ iliyowavutia wengi Afrika Mashariki lakini waliachana Novemba 2014 baada ya kuwepo tuhuma za kuchepuka kutoka kila upande.