Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa mahojiano mafupi aliyofanya na Jamii Production kabla ya KUZINDUA RASMI shughuli za kutayarisha na kusambaza matangazo ya Radio na Video.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwa na waanzilishi wa Jamii Production, Mubelwa Bandio (kulia) na Abou Shatry (kushoto)
Naam....
Kwa baraka za Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, JAMII RASMI IMEZINDULIWA RASMI Oktoba 26, 2013, alipotutembelea kuangalia utendaji wetu na kuizindua rasmi hapa ofisini kwetu Washington DC.
Hii ilikuwa ni ZAIDI YA TUKIO.
Ilikuwa ni BARAKA KWETU na tunamshukuru kila aliyewezesha hili.
NA SASA.....
Kazi ya kutekeleza yale yaliyousiwa na Mhe Waziri, yaliyo yaliyo msingi wa kituo chetu, yale yaliyo MAHITAJI ya walaji (hadhira yetu) NA WAJIBU WA FANI YETU ndio imeanza.
Na......
Hakuna litajalokuwa na maana kama hatutajua namna ambavyo utendaji wetu unaathiri maisha yako kwa namna CHANYA na HASI
Wewe (msikilizaji, mtazamaji na msomaji wetu) ni mdau mkubwa wa kufanikisha hili.
Tuzidi kushirikiana
TWAWAPENDA
Mhe. Waziri Dkt Fenella Mukangara na Afisa Habari katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mindi Kasiga pamoja na wanaJAMII
Bwn Isidory Lyamuya akipata mkono wa pongezi toka kwa Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production