mzee wa upako
POLISI WA INTERPOL WATUMI KA
Mzee wa Upako anaendelea kufunguka: Siku mbili mbele wakaja wengine, wakasema wao ni Polisi wa
Kimataifa (I nterpol). Nao wakasema wamekuja kunipekua, lakini wao licha ya kutokukuta chochote
walinikamata na kunipeleka Mahabusu ya Gereza la Keko, D ar ambapo nilikaa kwa muda wa kama wiki
mbili.
AZITAJA SIKU ZA MAJARI BU
Mzee wa Upako: Hakika zilikuwa ni siku za majaribu kwangu kukamatwa kwa tuhuma za kuj ihusisha na
biashara ya madawa ya kulevya, lilikuwa ni jambo ambalo sijawahi kulifanya achilia mbali kuliwaza.
Licha ya kukaa kwa wiki mbili kule mahabusu, Polisi wa I nterpol nao walij iridhisha kwamba mimi sifanyi
biashara hiyo, wakaniachia huru niendelee kumtumikia Mungu wangu.
AWAGUND UA WABAYA WAKE
Mchungaj i huyo maarufu kwa msemo wake WATASHINDANA, LAKI NI HAWATASHIND A aliendelea kusema
kuwa aligundua kukamatwa kwake kulitokana na mpango wa siri uliofanywa na baadhi ya wachungaj i
wenzake (hakuwataja maj ina) kwa aj ili ya kumdhoofisha kiimani.
“Zilikuwa ni mbinu chafu za kunidhoofisha kiimani kutoka kwa baadhi ya wachungaj i wenzangu wenye wivu
na huduma yangu. Lakini kwa j ina la Yesu aliye hai walishindwa, watashindana lakini hawatashinda,”
alisema Mzee wa Upako.
AHISI KUOND OLEWA HADHI
Mzee wa Upako alisema tukio hilo aliliona kama la kumwondelea hadhi katika jamii, hususan kwa waumini
wake lakini kwa kuwa yeye ni ‘super charge’ kamwe hawezi kuruhusu imani yake iyumbishwe na hila za
muovu shetani.
ANACHOMS HUKURI A MUNGU
Mchungaj i huyo alisema baada ya kutoka Keko alimshukuru Mungu kwa vile hakuna chombo chochote cha
habari kilichofuatilia juu ya sakata hilo na kwamba gazeti hili (Risasi Jumamosi) linakuwa la kwanza
kuandika.
“Nashukuru hakuna chombo chochote cha habari kilichogundua juu ya habari hiyo, ninyi mnakuwa wa
kwanza kuijua na hata kuiandika kama mtapenda,” alisema Mzee wa Upako.
APINGA DHANA YA WATUMI SHI WA MUNGU KUUZA UNGA
Akizungumzia kwa undani sakata la watumishi wa Mungu kuj ihusisha na biashara ya unga, Mzee wa Upako
alisema:
“S iamini kama kweli kuna watumishi wa Mungu wa hapa Tanzania wanafanya biashara hiyo. Kinachotokea
ni kwamba, watu wamekuwa wakiwasingizia watumishi kwa sababu zao.”
WAUMINI WAKE SASA
Juzi Alhamisi, Risasi Jumamosi liliwasiliana na baadhi ya waumini wa kanisa hilo ambapo walisema
mtumishi wao huyo amekuwa akionewa kij icho kutokana na mafanikio yake ya kiroho na kimwili.
“S isi waumini wa GRC tukisikia lolote baya kuhusu Mzee wa Upako huwa hatushtuki kwa sababu wapo
baadhi ya watumishi wa Mungu wanamuonea kij icho kwa sababu ana mafaniko ya kiroho na kiimani,”
alisema muumini mmoja bila kutaja j ina.
Mwingine alisema nguvu kubwa ya kiroho aliyonayo mtumishi huyo imemfanya aibue maadui wasio na hofu
ya Mungu kwa kumpakazia skendo mbalimbali wakiamini akichafuka waumini watamkimbia.
Jumatano iliyopita, paparazi wetu alifika Kituo Kikuu cha Polisi (Police Central), D ar na kuulizia ishu hiyo
ambapo afande mmoja alisema anayeweza kujua ni I GP Mstaafu, Omary Mahita ambaye wakati huo alikuwa
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya
Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ziligonga mwamba kufuatia simu yake ya kiganjani kutokupatikana
hewani
chanzoBONGOCLAN.COM