Moto ukiendelea kuwaka katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Grace Lodge iliyoko katika maeneo ya Kitanzani katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.2. Moto ukiwaka kwa ndani ya nyumba ya kulala wageni ya grace lodge.3. Wananchi wakishangaa moto ukiendelea kuwaka katika nyumba ya kulala wageni ya Grace Lodge uliotokea juzi maeneo ya Kitanzani katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.(Picha zote na Denis Mlowe)
NYUMBA KULALA WAGENI YAUNGUA MOTO
Na Denis Mlowe,Iringa
MOTO mkubwa ambao chanzo chake hakijajulikani uliibuka juzi na kuteketeza nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Grace Lodge na kusababisha hasara ya shilingi milioni 225.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi amethibitiisha kutokea kwa moto huo na uliosababisha hasara kubwa kwa mmiliki wake Jerida Jackson, Mungi alisema chanzo cha moto huo hakijajulikana na hakuna madhara kwa binadamu zaidi ya mali iliyoko katika nyumba hiyo.
Mungi alisema jeshi la polisi liko katika uchunguzi kwa kushirikiana na shirika la umeme Tanzania (Tanesco) kuweza kubaini chanzo cha moto huo na madhara mengine yaliyojitokeza baada ya kuteketea kabisa.
Nyumba hiyo iliyoko maeneo ya Kitanzani katika halmashauri ya manispaa ya Iringa inamilikiwa na Jerida Jackson (32) ambaye alizungumza na Tanzania Daima kuwa thamani ya vitu vilivyoteketea ndani ya nyumnba hiyo ni zaidi ya Sh 225 milioni huku akifafanua kuwa alipata taarifa za kuungua nyumba yake kutoka kwa mmoja wa wahudumu waliokuwa wakifanya kazi katika nyumba hiyo.
Huku akibubujiwa na machozi alisema (Sijui kitu mimi kuhusu chanzo cha moto huo sina cha kusema,lakini kumekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme tangu Jumatat na hata jana (juzi) kulikuwa na tukio hilo lakini sijui kama hicho ndicho chanzo ama la”alisema Jackson.
Katika hatua nyingine wakazi mkoani hapa wamelitupia lawama jeshi la Zima moto Mkoa wa Iringa wakidai limechelewa kufika eneo la tukio kuuzima moto na ndio sababu ya nyumba hiyo kuteketea.
Mmoja wa wananchi hao Hadija Ramadhani alisema tukio la kuchelewa kwa gari hilo ndiko kumechangia mto kuunguza sehemu kubwa ya nyumba hiyo. Naye Joseph Chengula alisema kikosi cha zima moto kilitumia gari dogo ambalo halikuwa na uwezo wa kuzima moto.
“Mara ya kwanza wamekuja na gari dogo ambalo halikuwa na uwezo wa kuzima moto huu,limeishiwa maji na hii sasa ni mara ya tatu linarudia kama wengetumia hili kubwa lkilifika muda huu ni dhahiri moto usingeangamiza nyumba kwa kiwango kikubwa hivi. Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kitanzini Jesca Msambatavangu alipengeza ushirikiano ulioonyeshwa na wananchi wakati wa kuzima moto huo ambao walikuwa wakitumia ndoo kuchota maji na kubwagia maeneo yaliyoathirika.
Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kenned Komba alitetea kitendo cha skari kuchelewa eneo la tukio akidai limetokana na taarifaza mto kuchelew akufika ofisini kwake.
“Tunayo namba ya 114,kazi yake ni kupata taarifa za matukio toka popote yanapotokea lakini kwa leo haikutumika,tumeletewa taarifa na watu waliokuja na pikipiki tu,lakini pia gari letu kubwa lilikuwa gareji ndio sababu tumetumia gari ndogo ambayo mafuta maji yaliyopo huisha ndani ya muda mfupi”alisema Komba.
Komba alisema hata hivyo kazi waliyoifanya ni kubwa kwani baadaye walipeleka magari yote eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima moto huo