Wastara Juma akiwa na simanzi wakati wa dua maalum ya kumbukumbu na kumuombea mumewe.
Stori: Brighton Masalu na Deogratius Mongela
DUA maalum ya kumbukumbu na kumuombea aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, Marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ imezua minong’ono mingi kufuatia wasanii wengi wanaounda Kundi la Bongo Movie kudaiwa kumfanyia mbaya mkewe, Wastara Juma kwa kutohudhuria, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.
Wastara akilia wakati wa kumbukumbu ya mumewe.
Kwa upande wake, Wastara alisema anamshukuru Mungu kwa kufanikisha shughuli hiyo na kuwaombea kwa Mungu wote waliojitokeza kumuunga mkono kwenye dua hiyo.
“Nawashukuru wote waliojitokeza, wamenifariji sana,” alisema Wastara kwa simanzi.
Wasanii wa filamu waliohudhuria dua hiyo, ni pamoja na Denis Sweya ‘Dino’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Flora Mvungi, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ na Suleiman Bin Sinan ‘Bond’.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ alipotafutwa, simu iliita bila kupokelewa.
Sajuki alifariki dunia Januari 2, 2012 na katika kutimiza mwaka mmoja kaburini misa nyingine itafanyika nyumbani kwa wazazi wake mkoani Songea Januari 2, 2014.