MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Feb 12, 2014

WAFANYABIASHARA MWANZA WAGOMA TENA. JIJI LA MWANZA LAONEKANA KUWA KAMA KIJIJI HAKUNA HUDUMA KABISAAAA!!!!!!!

 Wadau mbalimbali wameonekana wakisota leo kuzisaka huduma na wasifanikiwe kuzipata.

 Wafanyabiashara wengine waliamua kwenda kupumzika kabisa majumbani mwao lakini wengine wakiwa pamoja na wafanyakazi wao wameonekana wakiketi nje ya maduka yao kusikilizia pengine kutakuwa na mabadiliko huku hasara ikiwasubiri.






 Ni wauza vocha na vyakula vidogo vidogo ndio wamebakia ingawa nao wanalalama kuwa hakuna wateja.


 Mtaa huu unao unga barabara za Lumumba, mitaa ya Shinyanga Hotel huwa na pilika za haja lakini leo pakavu mithili ya uwanja wa kandanda.

 Kufuatia mgomo huo athari kubwa  zimeonekana kwa sekta mbalimbali za huduma nyiginezo kudorora, kuanzia wadau wa vyombo vya usafiri kama daladala na tax ambao hutegemea pilikapilika za wachuuzi na wanunuzi kufanya huduma ya usafiri, hivyo kwa siku ya leo kipato chao kimeshuka kwa kiwango kikubwa.



 Siyo mitaa ya Liberty kunakojaa pilika pilika za biashara, siyo barabara ya Uhuru, Rwagasore, Lumumba wala Kenyata maduka maeneo yote yamefungwa hakuna biashara

 Mtaa wa msikiti wa ijumaa jijini Mwanza.



Mitaa ya barabara ya posta to Mwanza Hotel maduka yote ya wafanya biashra yalikuwa yamepigwa makufuli kufuatia mgomo huo ambao bado haijajulikana kuwa utakoma lini.