|
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akionyesha tofali la
kwanza la dhahabu kuzalishwa na mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji
cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. Wengine katika picha
kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe na
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO (shirika la
kwanza la kizalendo linalomiliki mgodi huo kwa asilimia 99) Balozi
Alexanda Muganda. |
|
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) pamoja na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe (kushoto)
wakionyesha tofali la kwanza la dhahabu kuzalishwa na mgodi wa STAMIGOLD
uliopo katika kijiji cha Marota kata ya
Kaniha wilayani Biharamulo. |
|
Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa STAMIGOLD akiongoza msafara wa Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwaonyesha shughuli
mbalimbali za uzalishaji mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha
Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. |
|
Baadhi
ya wafanyakazi wa mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota
kata ya Kaniha wilayani Biharamulo wakiwa katika eneo la uchimbaji
ambapo Waziri wa Nishati na Madini nchini amefanya ziara. |
|
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akipata maelezo katika
ramani ya eneo la uchimbaji mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha
Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. |
|
Eneo la uchimbaji mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. |
|
Uchimbaji ukiendelea. |
|
Shughuli za uchimbaji zikiendelea. |
|
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akipata maelezo kwa kina. |
|
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongoza msafara
kuelekea eneo lililoandaliwa maalum kwaajili ya Hafla ya kusherehekea
uzalishaji tofali la kwanza la dhahabu katika mgodi wa STAMIGOLD. |
|
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. |
Tanzania
inatarajia kuanza kunufaika na madini ya dhahabu baada ya Serikali kuamua
kuanza kuchimba madini hayo katika mgodi wa STAMIGOLD uliopo wilayani Biharamulo
mkoani Kagera.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa tofali la kwanza la dhahabu katika mgodi wa STAMIGOLD, Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa uchimbaji huo
utasaidia kuongeza ajira kwa watanzania.
Profesa
Muhongo ameongeza kuwa hatua hiyo itaondoa malalamiko yanayotolewa na baadhi ya
wananchi kuwa rasilimali nyingi nchini zinawanufaisha watu kutoka nje badala ya
watanzania.
|
Kaimu Meneja wa kampuni ya STAMIGOLD Dennis Sebugwao. |
Kwa upande
wake Kaimu Meneja wa Kampuni ya STANGOLD
Dennis Sebugwao amesema kuwa Kampuni ya STAMIGOLD ambalo iko chini ya Shirika la Madini STAMICO
inamiliki mgodi huo kwa asilimia 99 huku asilimia 1 ikimilikiwa na Hazina.
Shughuli za
uchimbaji wa dhahabu kwa mgodi huo zilianza mnamo tarehe 2 mwezi julai mwaka
huu, huku uendeshaji na shughuli zote za usimamizi na uzalishaji zikifanywa na Watanzania
wenyewe.
Pamoja na mafanikio tuliyonayo bado zipo changamoto mbalimbali zinazoukabili mgodi wetu.
-Kuyumba kwa bei ya dhahabu.
-Tunakabiliwa na
ufinyu wa mtaji wa kuendesha shughuli mbalimbali za mgodi huu. Mfano,
baadhi ya vitu vinavyohusiana na uzalishaji vingihavipatikani hapa
nchini hivyo tunalazimika kuvinunua nje ya nchi kwa gharama kubwa.
-Wavamizi wa mali mbalimbali za mgodi.
-Uhaba wa maji-
Tunategemea vyanzo vya maji kutoka Mto Muhama na Isozibi ambavyo
havitoshelezi kutokana na matumizi yaliyopo. Mito hii maji yake
hutiririka wakati wa mvua tu.
-Ukiritimba katika kupata vibali mbalimbali vinavyohusiana na shughuli za uendeshaji wa mgodi.
-Tupo katika eneo la
pembezoni mwa huduma za kijamii hivyo kusababisha kwenda umbali mrefu
kwaajiliya kupata baadhi ya huduma za kijamii mfano huduma za matibabu,
huduma za kibenki nk.
-Ushindani na makampuni
ya madini na hasa makampuni yenye majina makubwa katika kubakiza
wafanyakazi wenye utaalamu mkubwa kwani kumekuwa na tabia ya
kunyang'anyana wafanyakazi wenye utaalamu na ujuzi wa muda mrefu katika
vitengo mbalimbali.
|
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO (shirika la kwanza la
kizalendo linalomiliki mgodi huo kwa asilimia 99) Balozi Alexanda
Muganda. |
Matarajio yetu ni kuwa Mgodi wa kwanza utakaozalisha dhahabu kwa kiwango
kikubwa na gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu ya
Tanzania. Stamigold Company Limited ina matarajio ya kuzalisha dhahabu
yenye kiwango cha juu kwa gharama itakayowezesha kuongezeka pato la
Taifa kwa muda mrefu wa biashara hii, wakati huo huo kuongeza nafasi za
ajira kwa Watanzania na kuvutia washika dau kwa ajili ya maslahi ya
taifa zima.
|
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe akihutubia katika hafla
ya kuzalisha tofali la kwanza la dhahabu mgodi wa STAMIGOLD uliopo
katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. |
|
Baadhi
ya wafanyakazi katika hafla ya kuzalisha tofali la kwanza la dhahabu
mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika kijiji cha Marota kata ya Kaniha
wilayani Biharamulo. |
|
Wadau wa mgodi. |
|
Ni meza nyingine walipoketi wadau. |
|
Wageni
toka mashirika na taasisi mbalimbali wamealikwa kwenye hafla hii ya
kuzalisha tofali la kwanza la dhahabu mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika
kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. |
|
Wageni. |
|
Mc wa hafla hiyo. |
|
Wakuu
wa idara mbalimbali katika pozi wakifuatilia yanayojiri kwenye hafla ya
kuzalisha tofali la kwanza la dhahabu mgodi wa STAMIGOLD uliopo katika
kijiji cha Marota kata ya Kaniha wilayani Biharamulo. |
|
Sehemu ya wafanyakazi mgodi wa STAMIGOLD. |
|
Kwa umakiiini.... |
|
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifurahia zawadi ya picha aliyokabidhiwa na mgodi wa STAMIGOLD. |
|
Burudani.... |
|
Ngoma inogile. |
|
Picha ya pamoja. |
|
Kaimu Meneja wa kampuni ya STAMIGOLD Dennis Sebugwao (kulia) akimsindikiza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kutoka eneo la hafla ambapo kushoto (mwenye tai nyekundu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe |