MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Sep 3, 2014

Angelina Jolie na Brad Pitt wauza picha zao za harusi kwa shilingi bilioni 3.3

£££EMBARGOED UNTIL SATURDAY 11TH AUGUST
Kanye West na Kim Kardashian walikataa kuuza picha zao za harusi lakini si kwa Angelina Jolie na Brad Pitt. Mastaa hao ambao kwa pamoja hujulikana kama Brangelina wameuza picha zao za harusi kwa dola milioni 2, ambazo ni zaidi ya shilingi
bilioni 3.3 za Tanzania. Kiasi hicho cha fedha kimepatikana baada ya kulipwa na majarida mawili ya People na Hello!, wiki moja baada ya kufunga ndoa Aug. 23 nchini Ufaransa.
article-2190113-14975994000005DC-209_634x407
Hiyo sio mara ya kwanza Pitt, 50, na Jolie, 39, wameingiza fedha kutokana na maisha yao binafsi licha ya kuwa na maisha ya usiri. Wawili hao wala hawana msemaji wao.
Mwaka 2006, waliuza picha za kwanza za mtoto wao wa kike, Shiloh kwa jarida la People kwa dola milioni 4.
Mwaka 2007, Jolie na Pitt walifanya kazi na People na Hello!, tena kwa kuuza picha za kwanza za mtoto wao wa kiume, Pax kwa kiasi ambacho hakikujulikana.
Mwaka 2008, walidaiwa kulipwa dola milioni 14 na jarida la People kuchapisha picha za kwanza za watoto wao mapacha, Vivienne Marcheline na Knox Leon. Kwa pamoja wawili hao wana utajiri wa dola milioni 385.