Hitmaker wa Lofa Top C, amemaliza malumbano yaliyokuwa yakiendelea kati yake na uongozi wa Candy n Candy Records ya nchini Kenya, kutokana na uongozi huo kushindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba wao. Top C amesema makubaliano waliyoyafikia na menejimenti yake hiyo ni maslahi ya mapato ya nyimbo zake, kufanyiwa promotion, kurekodi nyimbo na kuzifanyia video pamoja na kuandaliwa show
.
“Walinipigia simu tukafanya maongezi, wamekubali kunifanyia nitakavyotaka, kama mkataba unavyosema hivyo wamehitaji nirudi kwenye kampuni na nilitakiwa niwe nimekwenda Nairobi lakini nilikuwa na matatizo ya kifamilia kwa hiyo mwezi wa tisa nitakuwa huko kuendelea na shughuli za kimuziki chini yao,” Top C aliiambia Bomba FM ya Mbeya.
“Nipo mbioni kuachia video ya wimbo wangu wa Nihurumie hivi punde chini ya usimamizi wao, lakini pia kuna ngoma nyingine itafuata itaitwa Kisura, ambayo mpenzi alitoka home Tanga kuja Dar es salaam kunitafuta mwisho wa siku hakunikuta mimi sikuwepo akapangishiwa ghetto na wanawake wenzake na kuanza kutumikishwa katika biashara ya ngono,” aliongeza.