
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akifuatana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Comoro Mohamed Ali Soilihi
katika uwanja wa Ndege wa Comoro wakati Dk.Shein alipomaliza ziara yake
ya siku nne nchini Comoro.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Viongozi wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Comoro katika Uwanja wa Ndege wa Comoro baada ya
kumaliza Ziara ya siku nne kwa mualiko wa Serikali hiyo.Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.