MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Sep 25, 2014

KAMPUNI YA SUPER MEALS LTD WASAMBAJI WA MAJI YA COOL BLUE YASHIRIKI MAONYESHO YA HOME EXPO JIJINI DAR

‎Kampuni ya Super Meals Ltd- watengenezaji wa maji ya kunywa ya Cool Blue wiki iliyopita waliweza kushiriki katika maonyesho ya Home Expo yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Baada ya Kajunason Blog kutembelea banda lao iliweza kujifunza mambo mengi likiwemo jinsi wanavyozalisha maji pamoja na usambazaji wake. Kikubwa zaidi kampuni hiyo kwa sasa imekuwa na kuanza kujizolea watumiaji wengi zaidi. Pichani kulia ni Afisa Mahusiano Khadija Amri akitoa maeelezo machache kwa mmoja ya wateja walioweza kufika kujionea bidhaa zinazozalishwa na makuni hiyo.
Maelezo yakiendelea.
Mteja baada ya kuridhika na maelezo aliweza kuweka kumbukumbu zake katika daftari la wageni.
Muoneano wa banda la Cool blue.
Bidhaa zinazozalishwa na Super Meals Ltd- watengenezaji wa maji ya kunywa ya Cool Blue