Kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Papakiny Kaai akitoa neno la
shukrani kwa uongozi wa NMB baada ya kupokea msaada wa madawati sabini
kwaajili ya shule za msingi zilizopo Loliondo
Meneja wa kanda
ya Kaskazini Bi.Vicky Bishubo akimkabidhi msaada wa madawati Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Papakiny Kaai kwa
ajili ya shule za msingi za Loliondo.Kulia ni Meneja wa Huduma kwa
wateja katika tawi la NMB Loliondo Bw. Abraham Mbise.
Na Mwandishi Wetu.
Huo ni
mwendelezo wa Benki katika kuchangia huduma za kijamii kwa njia ya
kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kwa wananchi na kuifanya benki
kuwa karibu Zaidi na watanzania.
Meneja wa NMB
kanda ya Kaskazini Bi Vicky Bishubo alisema msaada huo ni mwitikio wa
NMB kusaidiana na wananchi pamoja na serikali katika kutatua changamoto
za uhaba wa madawati kwa wanafunzi wa wilaya ya Ngorongoro.
Nae Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Papakiny Kaai
aliishukuru benki ya NMB kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua
changamoto mbalimbali za wilaya ya Ngorongoro na taifa kwa ujumla hasa
katika elimu na afya.
picha habari na KAJUNASON BLOG/ WAMBURABABU BLOG