Mkurugenzi wa kituo cha elimu na michezo cha Alliance Academy ya jijini Mwanza, James Bwire akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na Uzinduzi wa Michuano ya Kombe la Afrika Mashariki la Alliance utakaofanyika kesho (ijumaa) uwanja wa CCM kirumba Mwanza. |
Uwanja ulioteuliwa kufanyika uzinduzi kwa michuano hiyo ni dimba la CCM
kirumba Mwanza, nayo fainali itachezwa tarehe 27 na 28 mwezi huu
Septemba 2014 katika viwanja vya Alliance Academy Mwanza vilivyo
kamilika mara baada ya maboresho kufanywa kwa hisani ya shirikisho la
soka nchini TFF.
Mkurugenzi wa kituo cha elimu na michezo cha Alliance Academy ya jijini
Mwanza, James Bwire amevishukuru vyombo mbalimbali vya habari nchini
ikiwemo Radio ya watu Clouds Fm kwa kutia hamasa kwa michuano hiyo kiasi
cha kusababisha timu mbalimbali hata zile zilizo nje ya nchi kuhamasika
kushiriki michuano hiyo.
Aidha wadhamini mbalimbali tayari wameanza wamejitokeza kusapoti
mashindano hayo, hali ambayo imetia hamasa katika matayarisho. Zaidi
Mratibu wa Mashindano ya Alliance East Africa Cup James Bwire
anatiririka juu ya maendeleo ya mashindano hayo.. (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)